SHUKURANI
Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijaalia uzima na afya njema katika kipindi chote cha kukamilisha utafiti huu. Pili, ninamshukuru msimamizi wa utafiti huu, Dkt Muhammed Seif Khatib ambaye alikuwa mwongozaji wa kazi hii na alifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa utafiti huu unamalizika katika hali ya ubora zaidi. Mwenyezi Mungu amlipe ujira mwema, Amina. Aidha, nawashukuru walimu wangu wote walionifundisha kozi za Fasihi ya Kiswahili ambao kwa kiasi kikubwa waliweza kupanua uelewa wangu ulionisaidia kukamilisha utafiti. Tatu, nawashukuru wazazi wangu Bi Fatma Almasi na Bwana Omar Rashid ambao mbali na kunileya na kunipatia elimu, walifanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa namaliza masomo yangu kwa mafanikio mkubwa. Mwenyezi Mungu awape umri mrefu na wenye afya njema katika maisha yao. Vilevile ninawashukuru ndugu zangu Rukaiyya Omar, Tauhida Omar na Ali Omar kwa kuonesha upendo wao wa dhati kwangu na kumlea mtoto wangu katika misingi bora wakati nikiwa masomoni. Nitakuwa mwizi wa fadhila iwapo sikumshukuru mume wangu mpenzi Bwana Mbarouk Nassor kwa kunivumilia pale nilipomwacha na upweke lakini bado kaendelea kunidhihirishia upendo wake kwangu katika kipindi hicho kigumu. Nne, ninawashukuru walimu na wanafunzi wenzangu, Mabwana Kassim Simai, Makame Pandu, Khamis Saleh, pamoja na Mabibi Zuleikha Abdallah, Bushura Khamis na Salama Omar kwa mashirikiano na kubadilishana mawazo juu ya tafiti zetu.
Rashid, Z (2021). Huzuni Katika Nyimbo Za Taarab Za Waimbaji Bi Fatma Issa Na Shakila Said. Afribary. Retrieved from https://tracking.afribary.com/works/huzuni-katika-nyimbo-za-taarab-za-waimbaji-bi-fatma-issa-na-shakila-said
Rashid, Zeyana "Huzuni Katika Nyimbo Za Taarab Za Waimbaji Bi Fatma Issa Na Shakila Said" Afribary. Afribary, 18 May. 2021, https://tracking.afribary.com/works/huzuni-katika-nyimbo-za-taarab-za-waimbaji-bi-fatma-issa-na-shakila-said. Accessed 05 Jan. 2025.
Rashid, Zeyana . "Huzuni Katika Nyimbo Za Taarab Za Waimbaji Bi Fatma Issa Na Shakila Said". Afribary, Afribary, 18 May. 2021. Web. 05 Jan. 2025. < https://tracking.afribary.com/works/huzuni-katika-nyimbo-za-taarab-za-waimbaji-bi-fatma-issa-na-shakila-said >.
Rashid, Zeyana . "Huzuni Katika Nyimbo Za Taarab Za Waimbaji Bi Fatma Issa Na Shakila Said" Afribary (2021). Accessed January 05, 2025. https://tracking.afribary.com/works/huzuni-katika-nyimbo-za-taarab-za-waimbaji-bi-fatma-issa-na-shakila-said