IKISIRI
Tasnifu hii inahusu Matumizi ya msamiati unaosawiri mazingira ya Kizanzibari
katika riwaya za Muhammed Said Abdulla. Msamiati ni jumla ya maneno
yaliyomo katika lugha. Hivyo, kwa mujibu wa utafiti huu maneno yenyewe
yalichunguzwa kupitia riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale, Duniani Kuna Watu na
Kosa la Bwana Msa. Uchunguzi huu ulilenga kuchunguza na kubainisha msamiati
huo na etimolojia yake pamoja na athari yake kwa wasomaji.
Sababu ya kuchunguza suala hilo lilitokana na mtafiti kuvutika na lugha ya utunzi
wa riwaya hizo. Shabaha ni kupunguza au kuondoa tatizo la kutofahamika maana
iliyokusudiwa kwa baadhi ya msamiati, hasa kwa wale ambao si weledi wa kucheza
na lugha hiyo.
Mbinu ambazo zilitumika kupata data ni udurusu wa maandiko, udodosaji na
mahojiano. Jamii tafitiwa katika uchunguzi huu ilikuwa ni ya Wazanzibari kwa kuwa
ndiyo jamii ya mtunzi wa riwaya hizo. Data za uwandani zilizopatikana kwao
zilichanganywa na zile za maktabani kupitia maandiko mbalimbali. Data hizi
zilihusishwa na nadharia ya uhalisia kuhusu upatikanaji wa etimolojia sahihi ya
msamiati unaosawiri mazingira ya Kizanzibari na matukio ambayo yamo katika
riwaya za mtunzi huyo ambayo yamekithiri msamiati huo.
Matukio ya uchunguzi huo yalibaini kuwa usawiri wa msamiati na mazingira ya
Kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla upo kwa kiwango kikubwa.
Usawiri huo ulibainika zaidi kupitia miktadha ya maisha ya Wazanzibari kijiografia,
kilugha, kisanaa na kiutamaduni. Aidha, msamiati uliobainika ulijikita katika
vipengele vya kihistoria (kupitia lugha ya Kiarabu na Kiingereza), kiutamaduni
(kupitia utamaduni wa dini ya Kiislamu), na kilahaja (kupitia vijilugha vya wakazi
wa Zanzibar). Hali hiyo imetoa athari kwa wasomaji ya kuvutika na uandishi wa
mtunzi huyo, kubaini historia na silika yake, kubaini umahiri wake wa matumizi ya
visawe, kubaini historia na athari ya Wakoloni, kutambulisha lahaja na utofauti wake
kimatumizi, kushajiisha matumizi ya msamiati uliopo hatarini kupotea, na kuathiri
watunzi wengine wa Zanzibar waliomfuatia. Pia matokeo ya uchunguzi huo yametoa
mchango mpya kwa kuorodhesha msamiati na asili zake katika riwaya hizo.
Said, S (2021). Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla. Afribary. Retrieved from https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla
Said, Saida "Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla. Accessed 25 Nov. 2024.
Said, Saida . "Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 25 Nov. 2024. < https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla >.
Said, Saida . "Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla" Afribary (2021). Accessed November 25, 2024. https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla