IKISIRI
Tasnifu hii ilijigeza katika kuchunguza matumizi ya utanzia katika riwaya pendwa za
Kiswahili ulinganisho wa riwaya za Ben Mtobwa na Hussein Tuwa. Ponera (2014)
anasema kuwa utanzia ni mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali
vizuavyo huzuni, masikitiko, jitimai na mateso kwa hadhira yake. Vipengele hivyo
huweza kujengwa na mateso, ugumu wa maisha, vifungo, mabaa kama vile njaa,
gharika, kimbunga, magonjwa, ulemavu (wa viungo au michakato ya mwili, pamoja
na ule wa mifumo ya mwili kama vile ugumba, utasa).
Mapitio yaliyotumika katika tasnifu hii yaligawanyika katika makundi mawili. Kundi
la kwanza, mapitio yanayohusiana na utanzia, na kundi la pili, mapitio
yanayohusiana na riwaya pendwa. Mbinu iliyotumika ni udurusu maktabani pamoja
na usaili. Maeneo yaliyotumika kukusanyia data ni Dodoma na Dar es Salaam.
Nadharia iliyotumika ni uhalisia ambayo huchunguza utokeaji wa matukio ambayo
huendana na hali halisi ya ulimwengu.
Matokeo ya tasnifu hii yanaonesha kuwa utanzia upo katika kazi mbalimbali za
fasihi yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Aidha, yanaonesha kuna aina tatu za
utanzia ambazo, ni utanzia wa kimwili, utanzia wa kisaikolojia na utanzia wa
kimaumbile. Pia, kuna vijenzi mbalimbali ambavyo vinaibua utanzia katika riwaya
teule na jamii kwa ujumla. Vilevile, matokeo ya tasnifu hii yanaonesha kuwa kuna
uhusiano wa moja kwa moja kati ya matukio ya kitanzia na matukio ya kifutuhi.
mpya wa kitaaluma katika fasihi ya Kiswahili kama ifuatavyo: Mosi, kubainika kwa
tofauti ya tanzia na utanzia. Pili, kuibuliwa kwa matukio ya utanzia ambayo
hujitokeza katika riwaya pendwa na si tamthiliya pekee. Tatu, kuibuliwa kwa aina
mbalimbali za utanzia zilizotumika na waandishi teule.
Shomary, K (2021). Matumizi Ya Utanzia Katika Riwaya Pendwa Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Ben Mtobwa Na Hussein Tuwa. Afribary. Retrieved from https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-utanzia-katika-riwaya-pendwa-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-ben-mtobwa-na-hussein-tuwa
Shomary, Kuruthumu "Matumizi Ya Utanzia Katika Riwaya Pendwa Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Ben Mtobwa Na Hussein Tuwa" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-utanzia-katika-riwaya-pendwa-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-ben-mtobwa-na-hussein-tuwa. Accessed 22 Nov. 2024.
Shomary, Kuruthumu . "Matumizi Ya Utanzia Katika Riwaya Pendwa Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Ben Mtobwa Na Hussein Tuwa". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 22 Nov. 2024. < https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-utanzia-katika-riwaya-pendwa-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-ben-mtobwa-na-hussein-tuwa >.
Shomary, Kuruthumu . "Matumizi Ya Utanzia Katika Riwaya Pendwa Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Ben Mtobwa Na Hussein Tuwa" Afribary (2021). Accessed November 22, 2024. https://tracking.afribary.com/works/matumizi-ya-utanzia-katika-riwaya-pendwa-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-ben-mtobwa-na-hussein-tuwa