IKISIRI
Tasinifu hii ilijikita katika kujadili mdhihiriko wa utanzia katika ushairi wa Kiswahili. Diwani zilizochunguzwa ni Kichomi na Dhifa. Dhana ya utanzia katika tasinifu hii imetumika kama mbinu bunilizi inayotumia vipengele mbalimbali vizuavyo huzuni, masikitiko, machungu, majonzi pamoja na maumivu ya mwili, roho na akili kwa hadhira. Utafiti umeongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha matukio ya utanzia yaliyodhihirika katika diwani teule, kufafanua dhima za matumizi ya utanzia katika diwani teule na kufafanua athari za matumizi ya mbinu ya utanzia kwa wasomaji kupitia diwani teule. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Data ambazo zimetupatia majibu ya tasinifu hii zilikusanywa toka kwa wataalamu wa fasihi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa njia mbili, usaili na uchanganuzi matini. Matokeo yaliyopatikana ni: kubainika kwa matukio ya utanzia katika diwani teule. Matukio hayo ni: hali ngumu ya maisha, ulemavu wa viungo, vifungo, maradhi, ukatili, majanga na vifo. Vilevile, tumebainisha dhima za matumizi ya utanzia katika kazi za fasihi. Dhima hizo ni: hujenga hisia za woga, hufikirisha, hujenga uhalisia wa maisha na kuibusha majonzi kwa hadhira lengwa. Utanzia kama mbinu ya utunzi huwa na athari hasi au chanya katika matumizi yake katika fasihi ya Kiswahili. Athari chanya ni pamoja na: kufikisha ujumbe, kuakisi uhalisia wa maisha, kuweka karibu msomaji na mwandishi na kuitafakarisha hadhira. Athari hasi ni: kupunguza wasomaji, ugumu katika kueleweka na huwapa wasomaji hali ya kukata tamaa kuhusu maisha. Kupitia tasinifu hii, wasomaji na wahakiki wataweza kufahamu sababu za waandishi kutumia utanzia katika kazi zao za kiutunzi. Halikadhalika, imeonesha namna mbinu hii inavyoweza kutumika katika kujenga maudhui, hasa katika utanzu wa ushairi. Zaidi, tasinifu imebainisha kwamba mbinu ya utanzia inaweza kutumiwa na washairi katika kujenga maudhui yao, tofauti na hapo mwanzo ambapo utanzia ulizoeleka kuonekana kwenye tamthiliya pekee.
MACHIMU, J (2021). Mdhihiriko Wa Utanzia Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Kichomi Na Dhifa. Afribary. Retrieved from https://tracking.afribary.com/works/mdhihiriko-wa-utanzia-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-kichomi-na-dhifa
MACHIMU, JOSEPHINE "Mdhihiriko Wa Utanzia Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Kichomi Na Dhifa" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://tracking.afribary.com/works/mdhihiriko-wa-utanzia-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-kichomi-na-dhifa. Accessed 25 Nov. 2024.
MACHIMU, JOSEPHINE . "Mdhihiriko Wa Utanzia Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Kichomi Na Dhifa". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 25 Nov. 2024. < https://tracking.afribary.com/works/mdhihiriko-wa-utanzia-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-kichomi-na-dhifa >.
MACHIMU, JOSEPHINE . "Mdhihiriko Wa Utanzia Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Kichomi Na Dhifa" Afribary (2021). Accessed November 25, 2024. https://tracking.afribary.com/works/mdhihiriko-wa-utanzia-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-kichomi-na-dhifa