IKISIRI
Utafiti huu unahusu kuchunguza mielekeo ya watumiaji lugha ya Kiswahili kuhusiana na
ukinzani katika methali. Kwa mfano methali, Fuata nyuki ule asali na Fuata nyuki ufe
mzingani. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili; nadharia ya mguso na nadharia ya
umaanishaji. Katika upande wa ukusanyaji data, utafiti huu ulitumia hojaji kwenda nyanjani
na udurusu wa kina kuhusu methali za Kiswahili. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kubaini na
kuchanganua mielekeo ya wanafunzi na walimu wa fasihi ya kiswahili kuhusu kuwepo na
methali ambazo maana zake zinakinzana. Matokeo yalibaini kwamba idadi kubwa ya
watafitiwa ina mwelekeo chanya kuhusiana na suala lililotafitiwa. Baadhi ya sababu
zilizochangia watafitiwa kuwa na mwelekeo chanya ni pamoja na maoni kwamba methali hizi
zilizo na maana kinyume humsaidia mwanajamii kutafakari kabla ya kuchukua mwelekeo
fulani na labda kuepuka matatizo ya baadaye. Mojawapo ya majukumu ya methali ni
kushauri. Hivyo basi, ukinzani utakupa nafasi ya kuchagua ushauri unaokufaa binafsi na upi
wa kutupilia mbali. Aidha, kila methali huwakilisha hali halisi ya maisha. Maisha yenyewe
yamejaa hali kinzani kama vile urafiki/uadui, wema/ubaya, furaha/huzuni na kadhalika. Kwa
kuzingatia kauli hii, kila methali huwakilisha hali fulani. Kwa mujibu wa baadhi ya
waliotafitiwa, ukinzani huleta mwelekeo hasi. Walitetea kauli hii kwa kusema kuwa methali
zinapokinzana huzua utata na hali ya kumchanganya mtumiaji lugha asijue methali gani
itamfaa kwani moja inakuongoza huku, nayo nyingine inakutuma kule! Utafiti huu ulibaini
kuwa walimu wana changamoto kubwa sana wanapoelezea maana na matumizi ya methali
zinazobishana kwa wanafunzi wao. Asilimia mia moja ya walimu wa fasihi waliotafitiwa
walitoa changamoto wanazokumbana nazo wanaposomesha suala la ukinzani katika methali
za Kiswahili. Ubishi upo katika methali za Kiswahili lakini iwapo kila methali itatumika
katika muktadha, hali na kwa hadhira mwafaka suala la ubishi huu halitakuwa changamoto
kubwa. Jambo la msingi litakalozingatiwa ni maana (ufaafu) na matumizi ya methali
mahususi. Nadharia ya umaanishaji inashikilia kuwa fasihi inapaswa kuwa na maana. Maana
itapatikana baada ya kutumia kila methali katika muktadha na mazingira mwafaka, ndiposa
mguso au athari ya fasihi ipatikane (ili fasihi iweze kutekeleza jukumu lake katika jamii).
MBUSYA, C (2021). Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya. Afribary. Retrieved from https://tracking.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya
MBUSYA, CATHERINE "Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya" Afribary. Afribary, 08 May. 2021, https://tracking.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya. Accessed 09 Nov. 2024.
MBUSYA, CATHERINE . "Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya". Afribary, Afribary, 08 May. 2021. Web. 09 Nov. 2024. < https://tracking.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya >.
MBUSYA, CATHERINE . "Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Shule Za Upili Kuhusu Methali Kinzani; Uchunguzi Katika Kata Ya Kitui Mjini; Kaunti Ya Kitui; Kenya" Afribary (2021). Accessed November 09, 2024. https://tracking.afribary.com/works/mielekeo-ya-wanafunzi-wa-shule-za-upili-kuhusu-methali-kinzani-uchunguzi-katika-kata-ya-kitui-mjini-kaunti-ya-kitui-kenya