Ufasihi Katika Kasida Za Madrasa

IKISIRI

Huu ni

utafiti uliofanywa juu ya ufasihi katika kasida za madrasa kutoka wilaya ya

Mjini Zanzibar kwa mwaka 2013. Tafiti mbalimbali zimefanyika kabla ya utafiti huu,

lakini zote hizo zimeelezea maana ya kasida, historia na dhima ya jumla ya kasida

ambayo ni kumsi fu mtume Muhammad (s.a.w) mfano Simiyu (2011:89) na Mulokozi

2011:14) 14). Dhana hiyo pia ime elezwa kabla na BAKI ZA (2010:147), Paden (2009),

Tuzin (2009) Al Mubarakpuri (2004:310), Ntarangwi (2004:67) na Mulokozi

(1996:70 Kwa kuchunguza kwa undani tafiti hizi zote hazijaelezea ufasihi

unaojitokeza katika kasida za madrasa.

Madhumuni ya utafiti huu ni kuchunguza ufasihi unaojitokeza kati

ka kasida za

madrasa. Kama wasem avyo BAKIZA (2010:82) kuwa fasihi ni sanaa ya lugha.

Hivyo usanii wa kasida ni mbinu mbali mbali zilizotumika katika kasida za madrasa

zenye kudhihirisha ufundi au usanii wa lugha . Kwa mfano matumizi ya lugha, ujenzi

wa muundo, uteuzi wa mtindo na uibuaji wa dhamira.

Utafiti huu ni muhimu katika taaluma ya f

asihi simulizi hasa katika vipengele vya

fani na maudhui pamoja na kubainisha utendaji wa kasida za madrasa za wilaya ya

Mjini Zanzibar. Utafiti huu utawafaa wanazuoni wengine wanaotaka kufanya utafiti

zaidi kuhusu kasida. Matokeo ya utafiti huu ya takuwa k ianzio kwa yale masuala

ambayo hajashughulikiwa katika utafiti huu.

Mbinu shirikishi (kuangalia), mahojiano ya ana kwa ana na dodoso la maswali

zilitumika katika kukusanya data za utafiti huu. Hatimaye nadharia ya Ujumi wa

Kinudhuma ilitumika wakati wa kuw asilisha na kufafanua data za utafiti huu.